Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar kwa Ufupi
Historia โข Majukumu โข Dira โข Utekelezaji โข Idara
Afisi hii ilianzishwa na Waingereza mwaka 1914 baada ya Zanzibar kuwekwa chini ya Utawala wa Mahamia kwa mujibu wa Heligoland-Zanzibar Treaty (1890). Lengo kuu lilikuwa kutoa ushauri wa kisheria kwa Serikali ya Utawala wa Mahamia.
Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964, Serikali ya Mapinduzi iliendelea na Afisi hii kwa lengo la kutekeleza majukumu ya Mwanasheria Mkuu.
Kuiwakilisha Serikali na taasisi nyengine za umma katika kesi za madai.
Kuanzisha na kufanya mapitio ya sera zinazohusiana na uandishi wa sheria.
Kuandaa na kusimamia taratibu za utayarishaji wa miswada.
Kutoa huduma za kisheria kwa serikali katika mashauri ya madai, kibiashara na kimataifa.
Kutoa ushauri wa kisheria katika majadiliano na mikataba ya Serikali.
Kuratibu utoaji wa taarifa kwa taasisi za Serikali kuhusu mikataba ya kimataifa.
Kukusanya na kusambaza mikataba ya kimataifa na kikanda.
Kufanya tafiti na kupendekeza marekebisho ya sheria.
Kutoa mafunzo juu ya nyanja mbalimbali za sheria.
Kuchukua na kufanya mapitio ya sheria za Zanzibar kwa lengo la kuziendeleza na kurekebisha mifumo yake.
Dira: Kusimamia upatikanaji wa haki kwa wakati na utawala wa sheria kwa wote.
Dhamira: Kuhakikisha haki, usawa na utawala wa sheria kwa kutoa huduma bora za kisheria.
Kanuni za Maadili: Uwazi, uwajibikaji, ufanisi, ushirikiano, ubora wa huduma, utu, usawa na utaalamu.
Majukumu haya yanatekelezwa kupitia maeneo matano makuu:
Kutoa ushauri wa kisheria kwa Serikali na taasisi za umma.
Kushiriki na kusimamia mikataba ya kitaifa na kimataifa.
Kuiwakilisha Serikali katika kesi na mashauri ya madai.
Kutayarisha miswada ya sheria na hati nyengine za kisheria.
Kupitia sheria za Zanzibar kwa lengo la kuziendeleza na kurekebisha mifumo yake.
-
IDARA YA RASILIMALI WATU, UTAWALA NA MIPANGO
-
Ndg. Fatma Iddi Ally
Mkurugenzi,
Idara ya Rasilimali Watu, Utawala na Mipango.
-
-
IDARA YA USIMAMIZI WA KESI NA MASHAURI YA MADAI
-
Ndg. Said Salim Said
Mkurugenzi,
Idara ya Usimamizi wa Kesi na Mashauri ya Madai.
-
-
IDARA YA UANDISHI WA SHERIA NA SERA ZA KISHERIA
-
Ndg. Hassan Ali Haji
Mkurugenzi,
Idara ya Uandishi wa Sheria na Sera za Kisheria.
-
-
IDARA YA HUDUMA NA USIMAMIZI WA MIKATABA NA UHUSIANO
-
Ndg. Fatma Saleh Amour
Mkurugenzi,
Idara ya Huduma na Usimamizi wa Mikataba na Uhusiano.
-
-
IDARA YA MAPITIO NA UTAFITI WA SHERIA
-
Dkt. Abdul-Nasser Hikmany
Mkurugenzi,
Idara ya Mapitio na Utafiti wa Sheria.
-
-
AFISI YA MWANASHERIA MKUU PEMBA
-
Ndg. Massoud Nassor Moh'd
Afisa Mratibu,
Afisi ya Mwanasheria Mkuu Pemba.
-