Uandishi wa Sheria
Huduma ya Kuandaa, Kusahihisha na Kusimamia Nyaraka za Kisheria
Muhtasari wa Huduma
Huduma hii inahusisha kuandaa, kusahihisha na kutoa ushauri kuhusu nyaraka mbalimbali za kisheria ikiwemo miswada ya sheria, kanuni na matangazo mengine ya kisheria. Lengo kuu ni kuhakikisha sheria zinatungwa kwa usahihi na kuendana na mahitaji ya Serikali na wananchi.
Majukumu Makuu
Kuandaa Miswada ya Sheria na Matangazo ya Kisheria na kuchapisha katika Gazeti rasmi la Serikali.
Kutoa muongozo juu ya mfumo wa uandishi wa Sheria na Matangazo ya kisheria.
Kufanya mapitio ya Sheria na kuandaa majumuisho ya Sheria zilizorekebishwa.
Kufanya kazi yoyote inayohusiana na Uandishi wa Sheria.
Kutoa ushauri wa kisheria kwa Serikali.