SMZ Logo
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar - AGCZ

National Flag

Ujumbe Wa Mwanasheria Mkuu

Kutoka Afisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar


Mwanasheria Mkuu
Dkt. Mwinyi Talib Haji
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
Ujumbe Kutoka Afisi ya Mwanasheria Mkuu

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kufanikisha kuanzisha Tovuti yetu ya Afisi ya Mwanasheria Mkuu. Ninayo furaha kubwa sana ya kukamilika kwa Tovuti hii na kuweza kutumiwa na Taasisi mbali mbali za kisheria, wadau wa sheria pamoja na wananchi.

Lengo la kuanzisha Tovuti hii ni kuwawezesha wasomaji kupata taarifa mbali mbali za kazi za msingi zinazotekelezwa na Afisi. Kazi hizo zinahusiana na ushauri na usimamizi wa mikataba, usimamizi wa kesi, mapitio na utafiti wa sheria, miswada ya sheria, matangazo ya kisheria pamoja na sheria zote zilizounganishwa (consolidated laws) ambazo zitawawezesha wasomaji kuzisoma sheria hizo kwa urahisi na hivyo kuepusha kufanya marejeo ya sheria zilizofutwa au zilizorekebishwa.

Mwisho lakini si kwa umuhimu, napenda kuwahamasisha wanasheria wenzangu pamoja na wadau wote wa sheria, watendaji serikalini na wananchi kwa ujumla kuitumia Tovuti yetu ili kupata taarifa muhimu za Afisi na sheria kwa ujumla. Aidha, Afisi inawakaribisha kwa maoni na michango ili kuimarisha huduma zetu zinazopatikana kupitia Tovuti hii.

Kwa kumalizia napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa watendaji wa Afisi ya Mwanasheria Mkuu kwa kufanikisha kuandaa Tovuti hii kwa manufaa ya nchi.

Mwanasheria Mkuu.

Ahsanteni Sana,

Afisi ya Mwanasheria Mkuu

Zanzibar

โš™๏ธ Mpangilio

๐ŸŒ
Lugha
๐ŸŽจ
Muonekano
๐Ÿ”ค
Maneno